IQNA

Taasisi Ya Qatar yasambaza nakala 4,000 za Qur'ani zenye hati ya Braille

10:01 - October 17, 2017
Habari ID: 3471220
TEHRAN (IQNA)-Taasisi ya Misaada ya Qatar imesambaza nakala 4,000 za Qur'ani Tukufu zenye hati ya Braille ambayo hutumiwa na watu wenye ulemavu wa macho.
Taasisi Ya Qatar yasambaza nakala 4,000 za Qur'ani zenye hati ya BrailleNakala hizo za Qur'ani zimesambazwa miongoni mwa wenye ulemavu wa macho katika nchi mbali mbali zikiwemo Tunisia, Uturuki, Uingereza na Morocco.

Nakala hizo za Qur'ani ziki katika kifurushi kilichopewa jina la, 'Basirah Mushaf', na zimechapishwa kwa ushirikiano wa shirika moja la Malayasia.

Qur'ani hiyo yenye hati ya Braille pia ina kalamu ya kielektroniki yenye kuzungumza ambayo inawawezesha watumizi kuchagua na kusikiliza aya za Qur'ani. Aidha kifurushi hicho kinajumuisha pia qiraa ya wasomaji mashuhuri wa Qur'ani, maana ya ibara za Qur'ani, sababu za kuteremka sura n.k.

Tokea mwaka 2014, taasisi hiyo imesambaza nakala 6000 za Qur'ani Tukufu zenye hati za Braile kwa ajili ya wenye ulemavu wa machi katika mabara ya Asia, Afrika na Ulaya.

Nakala hizo maalumu za Qur'ani zenye hati ya Braille zimesambazwa Oktoba 15 kwa munasaba wa Siku ya Walemavu wa Macho.

/3652747

captcha