IQNA

Maonyesho ya Picha za Siku ya Arobaini ya Imam Hussein AS

TEHRAN (IQNA)-Maonyesho ya picha yanafanyika hapa Tehran, mji mkuu wa Iran kuhusu matembezi ya Arobaini ya Imam Hussein AS.
Maonyesho hayo ya siku 8 yanajumuisha picha 300 ambazo zilichukuliwa na mpiga picha Muirani Mujtaba Heidari katika matembezi ya Arobaini nchini Iraq katika miaka ya 2013, 2014, 2015 na 2016. Aidha kila usiku katika maonyesho hayo, kuna kundi la Iraq linaloandaa tamthilia ijulikanyao kama Taziye inayosimulia kisa ya kuuawa Shahidi Imam Hussein AS na wafuasi wake katika jangwa la Karbala.