IQNA

Khitma ya Sheikh Abdullah Jaqaf aliyekuwa mwalimu maarufu wa Qur’ani Somalia+PICHA

11:11 - October 22, 2017
Habari ID: 3471227
TEHRAN (IQNA)-Waislamu nchini Somalia hivi karibuni wameshiriki katika khitma ya Qur’ani Tukufu ya mwalimu maarufu wa Qur’ani nchini humo.

Marhum Sheikh Abdullah Muhammad, maarufu kama Abdullah Jaqaf, aliaga dunia mwaka 2009.

Tovuti ya alsomal.net imeandika kuwa, Sheikh Jaqaf alikuwa anaheshimiwa sana Somalia na alijulikana kwa ucha Mungu wake, maadili mema na jitihada za kustawisha Qur’ani katika jamii.

Alizaliwa mwaka 1915, katika eneo la Galguduud kati mwa Somalia na alianza kuhifadhi Qur’ani akiwa bado mtoto mdogo na kisha akaendelea na masomo ya Kiislamu. Akiwa na umri wa miaka 20 aliteuliwa kuwa mkuu wa madrassah ya kuhifadhi Qur’ani na akaendelea katika njia hiyo ya kuhudumia Qur’ani hadi mwisho wa umri wake uliojaa baraka.

Halikadhalika alikuwa na nafasi muhimu ya kustawisha amani na urafiki miongoni mwa watu wa matabaka na koo mbali mbali Somalia.

Idadi kubwa ya Waosmali walisoma na kuhifadhi Qur’ani katika chuo cha Marhum Sheikh Abdullah Jaqaf.


Khitma ya Sheikh Abdullah Jaqaf aliyekuwa mwalimu maarufu wa Qur’ani


Khitma ya Sheikh Abdullah Jaqaf aliyekuwa mwalimu maarufu wa Qur’ani


Khitma ya Sheikh Abdullah Jaqaf aliyekuwa mwalimu maarufu wa Qur’ani


Khitma ya Sheikh Abdullah Jaqaf aliyekuwa mwalimu maarufu wa Qur’ani


3654911

captcha