IQNA

Japan yawavutia watalii Waislamu kwa chakula halali

11:18 - October 23, 2017
Habari ID: 3471228
TEHRAN (IQNA)-Japan inaibuka kama nchi yenye watalii wengi Waislamu kutokana na huduma inazotoa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu hasa chakula halali.
Japan yawavutia watalii Waislamu kwa chakula halaliKwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, ingawa nchi hiyo tajiri kiviwanda ina idadi ndogo sana ya wakazi Waisalmu, lakini imechukua hatua imara kuwaandalia Waislamu mazingira mazuri ya kuishi na kutembea nchini humo. Katika maeneo kadhaa ya kitalii Japan hivi sasa kuna misikiti au vyumba vya swala, migahawa ya chakula halali na isiyouza pombe n.k.

Ongezeko la watalii Waislamu katika miaka ya hivi karibuni nchini Japan limeambanatana na kuongezeka idadi ya migahwa yenye kuuza chakula halali. Hivi sasa katika viwanja vya ndege na hoteli kubwa nchini Japan kuna migahawa yenye vyakula halali. Migahawa hiyo mbali na kupika chakula halali inapika vyakula maalumu kutoka nchi za Waislamu kama vile Bangladesh, Misri, Indonesia, Iran, Malaysia, Morocco, Pakistan na Uturuki.

Aidha Waislamu wanaOishi Japan wanaweza kununua nyama halali iliyochinjwa kutoka nchi za kusini wa Asia kama vile Indonesia au Malaysia. Kutokana na kuwa Uislamu ni dini ya pili kwa wingi wa wafuasi duniani sambamba na kuwa dini inayenea kwa kasi zaidi duniani, soko la bidhaa na huduma halali litaendelea kupanuka. Soko la bidhaa za Kiislamu lilikuwa na thamani ya dola trilioni 2.6 mwaka 2015 na linatarajiwa kuimarika zaidi huku Waislamu wengi wakiwa wanasisitiza kufuata mafundisho ya Kiislamu katika maisha yao ya kila siku. Kwa msingi huo, nembo ya ‘Halal’ itakuwa sehemu ya biashara nyingi hasa za vyakula, hoteli, benki, bima na masoko ya hisa.

3464226
captcha