IQNA

Mbunge wa Kwanza Mwanamke Muislamu achaguliwa Catalonia, Uhispania

10:56 - December 28, 2017
1
Habari ID: 3471328
TEHRAN (IQNA)-Eneo la Catalonia nchini Uhispania limepata mwanamek wa kwanza Muslamu mbunge katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi iliyopita na hivyo kufanya idadi ya wabunge Waislamu eneo hilo kuwa watatu.

Katika uchaguzi wa Disemba 21 ambao ulikuwa uchaguzi wa 12 wa Eneo la Mamlaka ya Ndani la Catalionia, vyama vinavyounga mkono uhuru wa eneo hilo kutoka Uhispania vimepata ushindi mkubwa.

Mbunge huo aliyechaguliwa ni Bi. Najat Driouech Mhispania mwenye asili ya Morocco na ambaye ana umri wa miaka 36. Amechaguliwa kwa tiketi ya chama cha Barcelona Republican Left Party of Caatalonia. "Nachukua nafasi hii katika wakati mgumu wa eneo la Catalonia na nataka kuifunza jamii kuwa hakuna raia wa daraja la pili," amsema Driouech ambaye alihamia Uhispania akiwa na wazazi waka wakati alipokuwa na umri wa miaka 9.

Kuna Waislamu 515,000 Catalonia mabao ni takribani asilimia 15 ya watu wote katika eneo hilo.

Inafaa kuashiria hapa kuwa Uhispania na Ureno ni nchi zilizokuwa zinatawaliwa na Waislamu kati ya miaka 711 and 1492 wakati huo eneo hilo likijulikana kama Al-Andalus. Katika karne ya 8 na 9 polepole sehemu kubwa ya Wakristo walipokea Uislamu uliokuwa dini tawala. Mnamo mwaka 1100 takriban 80% za wakazi walikuwa Waislamu.

3676816

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
هارون مصطفى
0
0
Maashaallah Alhamdulillah
captcha