IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Machafuko Iran yalipangwa na Marekani, utawala wa Kizayuni na nchi moja ya Kiarabu

15:16 - January 10, 2018
1
Habari ID: 3471349
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, ushahidi na nyaraka za kipelelezi zinaonesha kuwa machafuko ya hivi karibuni nchini Iran yalipangwa na pande tatu.

Ayatullah Ali Khamenei ambaye mapema Jumanne alikuwa akihutubia maelfu ya wananchi wa Qum waliokwenda kuonana naye ameeleza njama mbalimbali zilizofanywa na maadui kwa ajili ya kutumia vibaya malalamiko sahihi ya wananchi hapa nchini na kusema: Upande mmoja wa pande hizo tatu ni Marekani na Wazayuni ambao wamepanga machafuko hayo kwa miezi kadhaa na msingi wake ilikuwa kuanzia katika miji midogo hadi kwenye mji mkuu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, sehemu ya pili ya pande hizo tatu ni nchi moja tajiri ya Ghuba ya Uajemi ambayo imedhamini gharama za utekelezaji wa njama hiyo, na upande wa tatu ni vibaraka wa kundi la munafikina la MKO, na njama hiyo ilipangwa miezi kadhaa iliyopita.

Ayatullah Khamenei ameashiria pia baadhi ya maneno yanayosemwa katika vyombo vya habari vya maadui na kuongeza kuwa: Maadui walitumia vituo viwili katika nchi jirani kwa shabaha ya kubuni na kusimamia machafuko ya hivi karibuni hapa nchini; moja kati ya vituo hivyo kilikuwa na kazi ya kuongoza operesheni katika wavuti na cha pili kilisimamia machafuko; na vyote viwili viliongozwa na Marekani na Wazayuni na walikuwa na yakini ya kupata ushindi.    

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria nara zilizokuwa zikitolewa katika machafuko hayo na kusema: Moja kati ya nara hizo ni ile ya: "Hapana kwa ughali wa maisha", ambayo ni nara yenye mvuto iliyotolewa kuwashawishi baadhi ya watu kujiunga na machafuko, na awali baadhi ya watu walijiunga na nara hiyo lakini pale walipogundua kwamba nara hizo zinabadilika, walijitenga.

Ayatullah Khamenei amewaambia watawala wa Marekani kwamba: "Kwanza kabisa mumegonga mwamba katika matukio ya hivi karibuni hapa nchini na kama mtafanya hivyo tena katika siku zijazo hapana shaka kwamba mtafeli na kushindwa. Pili ni kwamba katika siku kadhaa zilizopita mumeisababishia hasara Iran na jambo hili halitapita hivihivi bila ya kulipiza kisasi, na tatu ni kwamba mtu huyu ambaye Wamarekani wenyewe wanasema ana matatizo ya kiakili na kinafsi anapaswa kuelewa kuwa, mchezo huu wa kiendawazimu hautapita bila ya kupewa majibu."

Itakumbukwa kuwa kuanzia Alhamisi 28 Disemba mwaka 2017, kwa siku kadhaa baadhi ya watu kwenye miji kadhaa nchini Iran walifanya mikusanyiko na maandamano ya kulalamikia masuala mbalimbali kukiwemo kutojulikana hatima ya watu waliopata hasara na kupoteza fedha zao katika taasisi za kifedha, ughali wa baadhi ya bidhaa na udhaifu wa serikali katika usimamiaji wa mambo ya nchi.

Hata hivyo baadhi ya maandamano hayo yalitumiwa vibaya na watu wenye nia mbaya na wahuni wanaoungwa mkono na baadhi ya nchi za Magharibi, za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel kuzusha fujo na machafuko.

Kufuatia fitina hiyo, tokea siku ya Jumatano wiki jana, wananchi wa Iran katika miji mbalimbali wamekuwa wakishiriki katika maandamano makubwa ya kulaani njama hizo za maadui na wahuni waliotumia vibaya fursa hiyo kuharibu mali za umma.

 

3677309

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bablee
0
0
Wamagharibi Hasa Wamarekani Ni Waenexaji Wa Fitna Tuuh
captcha