IQNA

Msikiti wa Stockholm wahujumiwa, wachorwa nembo za Kinazi

20:49 - January 21, 2018
Habari ID: 3471364
TEHRAN (IQNA)-Watu wasuijulikana wameuhujumu msikiti wa eneo la kati mwa mji mkuu wa Sweden, Stockholm Ijumaa usiku na kuchora nembo za kinazi.

Nembo hizi za kinazi zilibandikwa katika milango ya mbele ya Msikiti wa Sodermalm huku waliotekeleza hujuma hivyo wakiharibu mali za msikiti huo.

Imamu wa msikiti huo, Sheikh Mahmoud Khalfi amesema kumefanyika uharibifu mkubwa na kuongeza kuwa eneo la mbele na nyuma limeharibiwa.

Imamu huyo amesema kuwa msikiti huo umelengwa na wahalifu mara 22 mwaka 2017 na kuongeza kuwa hii ni mara ya tatu kwa msikiti huo kuchorwa nembe za kinazi ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2014.

Sheikh Khalfi amesema kamati ya msikiti kwa mara kadhaa imependekeza kuwekwa kamera za usalama msikitini lakini kuna baadhi ya watu wanaopinga wakisema eneo la ibada halipaswi kuwa na kamera kama hizo.

Katika miaka ya hivi karibuni Sweden imeshuhudia ongezeko la watu wenye misimamo ya kibaguz ya Kinazi kiasi cha kufanyika maandamano makubwa ya wanaounga mkono Unazi katika miji mikibuwa kama vile Stockholm na Gothenburg.

3465002

captcha