IQNA

Mashaindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanwake yaanza Tehran

23:23 - April 22, 2018
Habari ID: 3471476
TEHRAN (IQNA)-Kitengo cha wanawake katika Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Irna kimefunguliwa Jumamosi.

Kitengo hicho kimefunguliwa katika sherehe zilizofanyika hapa Tehran na kuhudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu akiwemo mkuu wa Shirika la Wakfu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambalo limeandaa mashindano hayo.

Bi. Maasouma Farzana, mkuu wa kamati ya wanawake katika mashindano ya kimatiafa ya Qur’ani ya Iran alihutubu katika sherehe hizo ambapo amesema kuna washiriki 28 waliohifadhi Qur’ani kikamilifu kutoka nchi 28 ambao wanashindano katika mashindano ya mwaka huu. Amesema jopo la majaji ni wataalamu 9 wa Qur’ani kutoka Iran na wengine watano kutoka nchi za kigeni. Amesema washindi watatunukiwa zawadi katika sherehe maalumu itakayofanyika Jumamosi.

Mashindano ya  35 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran mwaka huu yanajumuisha yale ya ya kawaida maalumu kwa ajili ya wanaume, na pia kutakuwa na mashindano mengine ya Qur'ani ya wanawake, ya wenye ulemavu wa macho, ya wanafunzi wa vyuo vikuu na ya wanachuo wa vyuo vya kidini.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran, ambayo yatafanyika katika miji mitatu ya Tehran, Mashhad na Qum, ni tukio kubwa zaidi linalohusiana na Qur'ani katika Ulimwengu wa Kiislamu na yamekuwa yakiimarika kila mwaka. Nara ya mashindano yam waka huu ni ‘Kitabu Kimoja Umma Mmoja.”

3707613

captcha