IQNA

Majina ya waliofika fainali ya Hifdi katika ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

22:27 - April 23, 2018
Habari ID: 3471478
TEHRAN (IQNA)- Jopo la majaji katika Mashindano ya 35 ya Kimatiafa ya Qur'ani ya Iran limetangaza majina ya waliofika fainali katika kategoria wanaume waliohifadhi Qur'ani kikamifliu katika mashindano hayo.

Kwa mujibu wa tangazo hilo waliofika fainali ni pamoja na  Ahsanullah Abu al-Hashem wa Bangladesh, Mostafa Esfehanian wa Iran, Mohammad Riyad al-Khaja wa Syria, Musa Ahmed Aala wa Mauritania, Muhammad Rashad Abdul Sami Aziz wa Misri , Aqil Khalil al-Batlat wa Iraq na Muhammad Ayyub wa Pakistan.

Waliofuzu watashindana Jumatatu na Jumanne katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA mjini Tehran.

Mashindano ya mwaka huu yaliyoafunguliwa rasmi Jumatano yanjumuisha Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran (ya kawaida maalumu kwa ajili ya wanaume) na pia kutakuwa na mashindano mengine ya Qur'ani ya wanawake, ya wenye ulemavu wa macho, ya wanafunzi wa vyuo vikuu na ya wanachuo wa vyuo vya kidini.

Mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani yanayofanyika kwa kaulimbiu ya "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja" sambamba na kuanza sherehe za mwezi huu mtukufu wa Shaaban yanawajumuisha wasomaji (quraa)   na waliohifadhi (hufadh)  Qur'ani  258 kutoka nchi 84 na yataendelea hadi tarehe 25 mwezi huu wa Aprili.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran, ambayo yanafanyika katika miji mitatu ya Tehran, Mashhad na Qum, ni tukio kubwa zaidi linalohusiana na Qur'ani katika Ulimwengu wa Kiislamu na yamekuwa yakiimarika kila mwaka.

 3708345

captcha