IQNA

Magaidi wavamiza gwaride katika mji wa Ahvaz kusini mwa Iran

20:44 - September 22, 2018
Habari ID: 3471685
TEHRAN (IQNA)- Magaidi wakufurishaji wanaopata himaya Uingereza na Saudi Arabia wameshambulia gwaride ya kijeshi katika mji wa Ahvaz kusini mwa Iran na kuua shahidi watu kadhaa wakiwemo wanawake na watoto.

Kundi la kigaidi na ukufurishaji la al-Ahvaziyah limetangaza kutekeza hujuma hiyo ya kinyama ambayo imelaaniwa kimataifa. Kundi hilo mwaka jana pia lilishambulia misafara ya watu wanaozuru maeneo ya kumbukumbu za vita, lilishambulia kwa risasi gwaride hilo kwa kuwalenga wananchi waliokuwa wakitazama maonyesho hayo ya kijeshi ambapo kutokana na shambulizi hilo watu kadhaa wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto wameuawa na kujeruhiwa.

Wakati huohuo Naibu wa Mkuu wa Mkoa wa Khuzestan wa masuala ya kisiasa na kijamii amesema watu 25 wameuawa shahidi na wengine 60 wamejeruhiwa kutokana na shambulio la kigaidi lililofanywa leo mjini Ahvaz.

Ali Hossein Hosseinzadeh aidha amethibitisha kuwa magaidi wanne waliofanya shambulio hilo wameangamizwa.

Kwingineko Rais Hassan Rouhani amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Ndani Abdoreza Rahmani Fazli na Mkuu wa Mkoa wa Khuzestan Gholamreza Shariati na kusisitiza kuchukuliwa hatuua kali kwa wahusika wa shambulio la kigaidi lililotokea mjini Ahvaz, mkoani Khozestan kusini magharibi mwa Iran.

Asubuhi ya leo limefanyika gwaride kubwa la vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC na vikosi vya jeshi la kujitolea la wananchi la Basij na vikosi vya jeshi la Polisi katika mikoa na miji mbalimbali nchini. Katika gwaride hilo ambalo limefanyika kwa munasaba wa ‘Wiki ya Kujihami Kutakatifu’,  vikosi hivyo vya ulinzi, vikiandamana na silaha na zana mbalimbali za kijeshi  vimeonyesha utayarifu wao wa kiulinzi.

Licha ya shambulizi la kigaidi lililofanywa mjini Ahvaz, kusini magharibi mwa Iran, gwaride la kufana la majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa mnasaba wa kuanza Wiki ya Kujihami Kutakatifu, limefanyika katika miji yote nchini.

3748769

captcha