IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Jinai ya Ahvaz ni mwendelezo wa njama za tawala vibaraka wa Marekani

20:59 - September 22, 2018
Habari ID: 3471686
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullha Sayyed Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kwa familia za mashahidi wa tukio chungu la hujuma ya kigaidi katika mji wa Ahvaz kusini mwa Iran leo asubuhi.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: Vyombo husika vya intelejinsia vina wajibu wa kuhakikisha vinachukua hatua haraka na kwa umakini kuwasaka wahusika waliosalia wa jinai hiyo na kuwakabidhi mikononi mwa vyombo imara vya mahakama nchini.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika ujumbe na salamu zake hizo za rambirambi, Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, amesema yuko pamoja na familia za mashahidi wa tukio hilo la kigaidi na akaziombea kwa Mola subira na utulivu pamoja na kupewa daraja juu waliouawa shahidi katika shambulio hilo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kuwa: Tukio chungu na la kusikitisha la kuuliwa shahidi wananchi kadhaa wa Iran huko Ahvaz na magaidi mamluki, limedhihirisha kwa mara nyingine ukatili na uhabithi wa maadui wa taifa la Iran.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa: Mamluki hawa wenye nyoyo katili wanaowamiminia risasi wanawake, watoto wadogo na watu wasio na hatia ni vibaraka wa watu walewale waongo na wazandiki wanaojidai kila mara kuzungumzia haki za binadamu, wakati nyoyo zao zilizojaa chuki haziwezi kuvumilia kuona nguvu na uwezo wa kitaifa unaoonyeshwa na vikosi vya ulinzi ya Iran.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamuu ameeleza bayana kwamba: Jinai za watu hao ni mwendelezo wa njama za tawala vibaraka wa Marekani katika eneo ambazo lengo lao ni kuvuruga usalama ndani ya Iran; hata hivyo watakufa na ndoto yao hiyo, kwani taifa la Iran litaendelea kushikamana na njia yake inayolipa heshima na utukufu, na kama ilivyokuwa huko nyuma litawashinda maadui zake wote.

3749065

captcha