IQNA

Rais Rouhani akihutubu katika Umoja wa Mataifa

Marekani imekiuka misingi na sheria za kimataifa kwa kujiondoa JCPOA

8:59 - September 26, 2018
Habari ID: 3471691
TEHRAN (IQNA)-Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya lran amesema Marekani ilikiuka sheria kinyume na misingi na sheria za kimataifa kwa kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran yaliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais Rouhani ameyasema hayo Jumanne alipohutubia mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani ambapo alibainisha kuwa, mapatano hayo ya nyuklia ya Iran maarufu kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utejelezwaji JCPOA yalipatikana kwa juhudi za kidiplomasia za zaidi ya muongo mmoja na mazungumzo mazito kwa ajili ya kuondoa mgogoro wa kubuniwa, na hiyo hatua ya Marekani kujiondoa katika maptano hayo ni kinyume cha sheria za kimataifa.

Akibainisha kwamba siasa ghalati za serikali ya Marekani kuihusu Iran zitaishia kufeli amesema kuwa, msimamo wa Tehran katika uga wa siasa za kigeni, umejengeka juu ya ushirikiano wa pande kadhaa na kufungamana na misingi iliyoainishwa na sheria za kimataifa.

Aidha Rais Hassan Rouhani amezungumzia propaganda za viongozi wa Marekani kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Iran na kuhoji kwa kusema: "Ni kiwango gani Iran inaweza kukitumia kufunga mkataba mpya na serikali ya Marekani isiyotekeleza ahadi?." Amefafanua kwamba, mazungumzo yoyote ni lazima yafanyike kupitia fremu ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA na chini ya azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, si kinyume na hivyo.
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya lran amesema kuwa siasa za Iran si za vita, si za vikwazo, si za vitisho wala si za kimabavu, bali ni ni za kutekeleza ahadi na kuheshimu sheria na kwamba, Tehran inaunga mkono amani na demokrasia katika eneo lote la Mashariki ya Kati.

Akizungumzia mapambano dhidi ya ugaidi katika eneo hili amesema, Wairan ambao jana na leo ni wahanga wa ugaidi, daima wamekuwa katika safu ya mbele ya mapambano dhidi ya janga hilo na wataendeleaza mapambano hayo. Rais Hassan Rouhani amezungumzia pia umuhimu wa kupanuliwa uhusiano mwema na majirani wa Iran na kuanzisha eneo la amani zaidi na lililostawi na kusema kuwa hicho ndicho kipaumbele kikuu cha siasa za kigeni za Iran na kusisitiza kwamba, mtazamo wa Iran ni wa kupenda amani kuhusiana na masuala mbalimbali ya kimataifa. Aidha amebainisha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kuihujumu au kuingia vitani na nchi yoyote.

3750205

captcha