IQNA

Nakala 5,000 za Qur'ani zasambazwa Malawi

13:54 - December 03, 2018
Habari ID: 3471759
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Masuala ya Kidini Uturuki (Diyanet) imesambazwa nakala 5,000 za Qur'ani Tukufu iliyotarujumiwa kwa lugha ya Kichewa nchini Malawi.

Kwa mujibu wa taarifa, nakala hizo zimekabidhiwa Waislamu wa nchi hiyo hasa wanafunzi.

Usambazwaji wa nakala hizo za Qur'ani umefanyika katika fremu ya mpango wa "Qur'ani Ni Zawadi Yangu" ambao umekuwa ukitekelezwa na Diyanet kwa lengo la kueneza ujumbe wa Qur'ani duniani.

Kwa msingi wa mpango huo nakala milioni moja za Qur'ani zilizotarjumiwa zitasambazwa katika nchi mbali mbali duniani.

Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa nchini Malawi ambao Waislamu wanakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 30 ya watu wote milioni 17 nchini humo.

3768893

captcha