IQNA

Mkutano wa kujadili 'Muamala wa Karne' katika IQNA

Kikao cha kujadili 'Nukta za Muamala wa Karne' ambao ni njama ya pamoja ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kilifanyika Julai 8 katika makao makuu ya Shirika la Habari la Qur'ani la Kimataifa, IQNA. Kikao hicho kilihudhuriwa na Balozi wa Palestina nchini Iran Salah al-Zawawi pamoja Hussein Sheikhul Islam, mwanadiplomasia mkongwe wa Iran ambaye pia ni mshauri wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu.