IQNA

Morocco, Nyota ya Africa

TEHRAN (IQNA) – Morocco, ambayo inajulikana pia kama Al Maghreb.

Hii ni nchi huru ambayo iko katika eneo la Afrika Kaskazini ambalo pia linajulikana kama Al Maghrib al Arabi Al Kabir. Morocco inapakana na Bahari ya Mediterranea upande wa kaskazini na Bahari ya Atlantiki upande wa maghribi. Aidhainapakana na Algeria upande wa Mashariki na Mauritania upande wa kusini. Mji mkuu wake ni Rabat na mji mkubwa zaidi ni Casablanca. Morocco iko katika eneo lenye ukubwa wa mita mraba 710,850 na idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 35. Morocco pia inadai umiliki wa eneo la Sahara Magharibi ambalo limekuwa likipigana kujitenga kwa miaka kadhaa sasa.

Baada ya Morocco kuondoka katika mamlaka ya utawala wa Baghaad wakati wa ufalme wa Harun al Rasid na kwa kuzingatia kuwa haikuwa chini ya utawala wa Uthmaniya, ilikuwa miongoni mwa nchi za Kiarabu zenye ustaarabu wa kipekee. Hatahivyo baadaye ilikoloniwa na Wafaransa na Wahispania na kisha ikafanikiwa kujinyakulia uhuru.

Dini rasmi Morocco ni Uislamu ambapo asilimia 99 ya wakazi wake ni Waislamu.