IQNA

Iran kusambaza nakala 3,000 za Qurani za Braille kwa wenye ulemavu wa macho

16:52 - October 07, 2019
Habari ID: 3472160
TEHRAN (IQNA) – Wenye ulemavu wa macho katika Jamhuri ya Kiislamu ya Irana watakabidhiwa nakala maalumu za Qur'ani zilizoandikwa kwa maandisi ya Nukta Nundu ama Braille.

Akizungumza na IQNA, afisa mwandamizi wa Shirika la Ustawi wa Jamii Iran Mohammad Nafariyeh amesema nakala hizo za Qur'ani zitasambazwa bila malipo kwa wenye ulemavu wa macho.

Amesema shirika hilo limetia saini mikataba na vyuo vya kidini kuchapisha vitabu kwa wenye ulemavu wa macho.

Nukta nundu ni muwasilisho wa herufi kwa njia inayoshikika au kutambulika kwa vidole ambapo herufi, namba na alama za kisayansi zinachorwa kiasi kwamba mwenye ulemavu wa macho, yaani asiyeona au mwenye uoni hafifu anaweza kutambua na kusoma kama kawaida.

Mbinu hii inatokana na mgunduzi wake Louise Braille kutoka Ufaransa ambaye aliigundua karne ya 19.

Ibara ya 2 ya mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu inataja nukta nundu kama mbinu muhimu kwenye elimu, uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, kupata taarifa na mawasiliano mbalimbali.

3847186

captcha