IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Iran itatoa pigo kwa maadui wanaoishinikiza na kuwalazimu kurudi nyuma

22:01 - June 27, 2020
Habari ID: 3472905
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, matokeo ya mashinikizo ya maadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu yatakuwa ni kuchezea kipigo maadui hao kutoka kwa taifa la Iran na kulazimika kurudi nyuma.

Iran itatoa pigo kwa maadui wanaoishinikiza na kuwalzimu kurudi nyumaAyatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo mjini Tehran wakati alipozunguza kwa njia ya video na mkuu na maafisa wa ngazi za juu wa Chombo cha Mahakama cha Iran na kusisitiza kuwa, kuna wajibu wa kulindwa nchi katika nyuga zote ikiwa ni pamoja na kukabiliana na uadui wa Marekani na Uingereza khabithi na pia kukabiliana na hatua zinazochukuliwa na nchi za Ulaya dhidi ya taifa la Iran. Amesema, kama tutatekeleza ipasavyo majukumu yetu, basi kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu njama zao zote zitafeli, watashindwa kufikia malengo yao na matokeo ya mashinikizo ambayo wenyewe wanajigamba kuwa ni ya kiwango cha juu kabisa yatakuwa ni kushindwa maadui hao na kuchezea kipigo kutoka kwa taifa la Iran na mwishowe watalazimika kulegeza misimamo yao na kurudi nyuma.

Ayatullah Khamenei pia amesema, njama kubwa zisizosita za maadui zinajaribu kuvuruga harakati yoyote ya marekebisho na mabadiliko katika mfumo wa Jamhuri ya Kisilamu ambapo maadui hao muda wote wanaeneza uvumi, kukatisha tamaa watu na kuwafanya wananchi wasiwe na mtazamo mzuri kuhusu mfumo wao wa utawala ili kuzuia mabadiliko na marekebisho hayo. Hata hivyo amesisitiza kuwa, njia pekee bora ya kukabiliana na njama zote zinazopiga vita mabadiliko ni kutofanya pupa, ni kusimama imara, ni kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na ni kuendelea kishujaa na njia hiyo ya mabadiliko.

Kiongozi Muadhamu amegusia pia matamshi ya rais wa Marekani aliyetishia kuwa watu wanaovunja nembo za utumwa na ubaguzi wa rangi nchini humo watafungwa jela miaka kumi  au uamuzi wa rais huyo wa kuwapokonya wakimbizi watoto wao na kusisitiza kuwa, kwenye filamu za nchi za Magharibi wanajaribu kuficha uhalisia wa mambo na wanaonesha kwamba wana mahakama zinazochunga uadilifu na hakuna dhulma katika jamii zao; wakati hiyo sio hali halisi ilivyo katika nchi za Magharibi.

3907099

captcha