IQNA

Harakati za Hamas na Fat'h zaahidi kuungana kukabiliana na utawala wa Israel

13:58 - July 03, 2020
Habari ID: 3472925
TEHRAN (IQNA) – Harakati za kupigania ukombozi wa Palestina za Hamas na Fat'h zimesisitiza kuhusu umoja wa kitaifa za Wapalestina ili kukabiliana na adui mvamizi na ghasibu pamoja, yaani Israel na njama zake ikiwemo ya 'Muamala wa Karne'

Saleh al Gharuri, naibu mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas na Jibril al Rajub, mkuu wa kamati kuu ya harakati ya Fat'h, wametangaza makubaliano waliyofikia kwa ajili ya kukabiliana kwa kila hali na mpango wa utawala wa Kizayuni wa kunyakua ardhi za Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. Viongozi hao wa Hamas na Fat'h walitoa tamko hilo katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari waliofanya hapo jana.

Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ulikuwa umepanga uanze kutekeleza siku ya Jumatano ya tarehe Mosi Julai mpango wake haramu wa kupora na kuunganisha asilimia 30 ya ardhi za Ufukwe wa Magharibi na ardhi zingine za Palestina unazozikalia kwa mabavu, lakini ukalazimika kuakhirisha na kusogeza mbele tarehe ya utekelezaji wake baada ya kushadidi mashinikizo ya upinzani ya Wapalestina na ya nchi mbali mbali duniani.

3471862

captcha