IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Jamhuri ya Kiislamu ni ubunifu muhimu zaidi wa Imam Khomeini (MA)

12:23 - June 04, 2021
Habari ID: 3473979
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema taifa la Iran leo na mustakabali wa mbali linapaswa kulinda kumbukumbu ya Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akihutubu moja kwa moja kwa njia ya televisheni kwa munasaba  wa kukumbuka mwaka wa 32 wa kuaga dunia Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kiongozi Muadahmu amesema ubunifu mkubwa zaidi wa Imam Khomeini ulikuwa ni Jamhuri ya Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa,  kazi kubwa aliyofanya Mtukufu Imam ilikuwa ni kubuni fikra na nadhari ya Jamhuri ya Kiislamu na kuingiza nadharia hiyo katika uga wa siasa na kisha hatimaye kutekeleza nadharia hiyo kivitendo.

Ameongeza kuwa, katika mifumo mbali mbali ambayo imeundwa duniani katika kipindi cha takribani karne mbili zilizopita, hakujashuhudiwa mfumo ambao umetabiriwa kustamabratika kama ilivyotabiriwa kuhusu Jamhuri ya Kiislamu. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wale waliochukizwa na mapinduzi hayo walikuwa wanatabiri kuwa yataanguka au kusambaratika baada ya miezi miwili n.k.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa mitazamo kama hiyo ilitokana na uzoefu wa mapinduzi katika maeneo mengine ambayo yalianza kwa nguvu lakini yakawa na mwiso mbaya.

Ayatullah Khamenei amesema siri ya kubakia na umashuri Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni maneno mawili, Jamhuri na Kiislamu yaani wananchi na Uislamu. Amefafanua zaidi kwa kusema maana ya Jamhuri ni wananchi na maana ya Uislamu hapa ni mfumo wa Kiislamu unaotegemea kura za wananchi. 

Kwingineko katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu ametilia mkazo udharura wa wananchi kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa rais na mabaraza miji na vijiji utakaofanyika Juni 18 nchini Iran. Amesema kuchagua mtu sahihi na anayefaa ndiyo njia ya kuondoa mapungufu na matatizo yaliyopo.

Ayatullah Ali Khamenei ameashiria sisitizo la Imam Khomeini la udharura wa kushiriki kwa wingi wananchi katika chaguzi mbalimbali hapa nchini, na kusema kuchagua mtu anayefaa na sahihi ndio suluhisho la mapungufu na matatizo mbalimbali. Ameeleza nukta muhimu zinazohusiana na udharura wa Rais ajaye wa Jamhuri kutekeleza uadilifu wa kijamii, kupambana ipasavyo na bila ya huruma na ufisadi na kuimarisha uzalisha na akasema kuwa: Wananchi wa matabaka yote wanapaswa kushiriki katika uchaguzi na kuwahamasisha wenzao kufanya hivyo.

Vilivile ameashiria kipindi cha awali cha baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na jinsi mabeberu wa kimataifa walivyokuwa wakitabiri kusambaratika mapinduzi hayo katika kipindi cha miezi miwili, 6 au mwaka mmoja na kusema: Kusimama kidete kwa Imam Khomeini, misimamo yake imara, ushindi mkubwa wa taifa katika vita na masuala mengineyo, yote hayo yalibatilisha utabiri wa mabeberu. Ameongeza kuwa baada ya kuaga dunia hayati Imam Khomeini maadui walikariri matarajio yao hayo ya kusambaratika Jamhuri ya Kiislamu. 

Ayatullah Khamenei ameashiria pia maendeleo na ustawi endelevu unaoshuhudiwa hapa nchini na kusema: Siri ya kubakia hai mfumo wa Imam Khomeini ni kuendelea kushikamana ka mambo mawili yaani Jamhuri (yani wananchi) na Uislamu. 

Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa, miongoni mwa kazi kubwa zilizofanywa na Imam Khomeini ni kubuni fikra ya Jamhuri ya Kiislamu na kuingiza fikra hiyo katika nadharia za kisiasa za kimataifa na hatimaye kutekeleza nadharia hiyo kivitendo.

 

3975570

captcha