IQNA

Wamorocco waanzisha kamepni ya kutaka mwakilishi wa Israel atimuliwe

15:56 - June 06, 2021
Habari ID: 3473982
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya watu wa Morocco wameanzisha kampeni katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kulaani jinai za kinyama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza huku wakitaka nchi yao ikato uhusino na utawala huo bandia.

Kwa mujibu wa gazeti la kimataifa la al Quds al Arabi wananchi wa Morocco wameanziska kampeni ya kutaka mwakilishi wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini humo David Govrin atimuliwe mara moja.

Kampeni hiyo ambayoe imezinduliwa katika mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter imewavutia maelfu ya Wamorocco.

Tarehe 22 mwezi Disemba mwaka jana Morocco na utawala haramu za Kizayuni wa Israel zilisaini mapatano ya kuanzisha uhusiano baina yao na kisha Marekani ikatambua rasmi mamlaka ya udhibiti wa Morocco kwa eneo la Sahara Magharibi. 

Morocco ni nchi ya sita ya Kiarabu baada ya Jordan, Misri, Imarati, Bahrain na Sudan  kuanzisha uhusiano kati yake na utawala ghasibu wa Kizayuni. 

Kitendo hicho cha Morocco cha kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel ambacho ni sawa na kusaliti malengo ya Palestina kimekabiliwa na radiamali hasi katika Ulimwengu wa Kiislamu na hata ndani ya Morocco kwenyewe. 

3975787

Kishikizo: morocco israel
captcha