Akizunguma na kanali ya televisheni ya Al Jazeera, amesema hakuna mazingira yoyote ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mwaka jana Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na kisha Morocco zilianzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel. Nchi zingine za Kiarabu ambazo zimeanzisha uhusiano na utawala bandia wa Israel ni Jordan na Misri huku Saudi Arabia ikiripotiwa kuwa na uhusiano wa siri na utawala huo haramu.
Kitendo hicho cha nchi hizo kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel ambacho ni sawa na kusaliti malengo ya Palestina kimekabiliwa na radiamali hasi katika Ulimwengu wa Kiislamu.