Hujjatul Islam Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukuruisha Madhehebu za Kiislamu ameyasema hayo katika mkutano wake Adel Bour, mwakilishi wa masuala ya kidini ya Uturuki nchini Iran.
"Kwa kweli kile ambacho wanasiasa wanakifuata katika nyanja ya kidiplomasia kinasababisha matatizo katika ulimwengu wa Uislamu," Shahriari alisema.
Aidha amesisitiza kuwa iwapo wasomi wa kidini watafuata mfumo thabiti, basi wanaweza kuchukua jukumu katika uwanja wa kisiasa.
"Dini kamwe haifuatii vita na ugaidi. Dini zote zinaheshimu maisha ya mwanadamu. Qur’ani Tukufu inasema kwamba anayemuua mtu mmoja kwa ni kana kwamba ameua ubinadamu wote."
Qur'ani Tukufu inalenga kuleta amani amani duniani, alisema, akitoa wito kwa wanazuoni kueleza masuala mbalimbali ya suala hili kwa jamii.
Kumekuwa na tafsiri mbalimbali za dini katika historia, alisema, akiongeza kuwa hii haipaswi kusababisha migogoro na iwapo hifilafu za kidini zitasababisha ugaidi na ukufurishaji, basi ni kinyume na kanuni za Kiislamu.
Shahriari pia alikosoa namna vyombo vya habari vinavyotumiwa kuvunjia heshima itikadi za wengine huku akitoa wito wa kudumishwa nidhamu wakati wa kutokubaliana.
Kwa upande wake, afisa huyo wa Uturuki aliashiria ulazima wa ukaribu kati ya madhehebu za Kiislamu.
3480599