IQNA

Waislamu Ufaransa

Mwanasiasa mwenye misimamo mikali ataka misikiti zaidi ifungwe Ufaransa

17:30 - October 05, 2022
Habari ID: 3475881
TEHRAN (IQNA)- Mwanasiasa mwenye siasa kali za mrengo wa kulia wa Ufaransa, Marine Le Pen amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Gérald Darmanin, kufunga misikiti zaidi ya Waislamu akisema kuwa kufungwa misikiti 24 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita haitoshi.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha BFMTV cha Ufaransa, Le Pen amesema kuwa Darmanin "anafunga msikiti hapa na msikiti pale... Ni lazima afunge misikiti yote yenye itikadi kali katika ardhi zetu." Amesisitiza haja ya kuwafukuza nchini Ufaransa Waislamu wote ambao amedai wanafuata matamshi ya itikadi kali.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, serikali ya Ufaransa imefunga misikiti 24 kati ya 99 ambayo imefuatiliwa kwa kisingizio cha "kupambana na itikadi kali".

Taratibu za kisheria bado zinaendelea kwa ajili ya kufunga misikiti mingi zaidi ya Waislamu kwa ombi la Waziri wa Mambo ya Ndani wa ufaransa.

Marine Le Pen ambaye alichuana na Rais Emmanuel Macron katika uchaguzi wa uraisi wa Ufaransa kwa tikiti ya chama cha kitaifa cha Rassemblement chenye siasa kali za mrengo wa kulia ameeleza pia upinzani wake dhidi ya vazi la hijabu la wanawake wa Kiislamu.

Le Pen, alisema katika kampeni za uchaguzi huo kwamba iwapo atashinda kiti cha urais, atapiga marufuku kuchinja wanyama kwa njia ya Kiislamu na vilevile vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu, hijabu.

3480733/

Kishikizo: ufaransa waislamu le pen
captcha