IQNA

Ugaidi Afrika

Hujuma za kigaidi ziliongezeka Afrika mwezi Septemba

11:47 - October 06, 2022
Habari ID: 3475886
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kimechapisha ripoti inayoashiria ongezeko la operesheni za kigaidi katika nchi za Afrika mwezi Septemba na kutaka kuongezwa hatua za kimataifa za kukabiliana na ongezeko la ugaidi katika bara hilo

Taasisi ya Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar ya Kufuatilia Itikadi Kali kimetoa ripoti kuhusu ongezeko la shughuli za kigaidi mwezi Septemba.

Kulingana na ripoti hiyo, idadi ya operesheni za kigaidi zinazotekelezwa na makundi magaidi wa wakufurishaji hasa  Daesh (ISIS), Boko Haram na Al-Shabaab, imefikia 54 katika mwezi uliopita, ikiwa ni ongezeko kubwa  ikilinganishwa na operesheni 45 zilizofanywa mwezi Agosti.

Operesheni hizo za kigaidi zimejumuisha milipuko ya mabomu, mauaji na mashambulizi kwenye vituo mbalimbali. Watu 251 waliuawa moja kwa moja katika operesheni hizo, 171 walijeruhiwa huku kukiwa na visa 129 vya utekaji nyara . Aidha mamia ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi hayo ya kigaidi.

Taasisi hiyo ya Al-Azhar imetaja sababu kuu ya kuongezeka kwa mashambulizi hayo ya kigaidi kuwa ni ushindani kati ya Al-Qaeda na Daesh barani Afrika na kushadidi migogoro ya kivita kati ya makundi hayo ili kupata rasilimali zaidi za kifedha. Kulingana na taarifa hiyo mashindano haya yatasababisha mzozo wa wazi kati ya Al-Qaeda na ISIS barani Afrika.

Taasisi ya Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar ya Kufuatilia Itikadi Kali limesisitiza kuwa kuhusu umuhimu wa kukabiliana na hatari na matokeo ya tatizo la ugaidi na itikadi potovu za kufurutu ada. Aidha taasisi hiyo imeseme bado nchi za Afrika hazicjachukua hatua za kukabiliana na mazingira ambayo yamepelekea kuibuka kushamiri makundi ya kigaidi barani humo.

Taarifa hiyo ya Al Azhar imesisitiza kuwa, iwapo jumuiya ya kimataifa na mashirika husika ya kimataifa hayatashughulikia haraka na kimsingi kuenea kwa ugaidi barani Afrika, jambo hilo litatishia amani na usalama wa kimataifa katika siku zijazo.

4089634

captcha