IQNA

Utawala wa Kizayuni wafungua tena Msikiti wa al-Aqsa

16:14 - October 31, 2014
Habari ID: 1465817
Utawala haramu wa Kizayuni, kwa mara ya kwanza leo Ijumaa alfajiri umefungua milango ya Msikiti wa al-Aqsa baada ya kuifunga mwaka 1967. Utawala huo pia umeshadidisha ulinzi katika maeneo ya jirani na msikiti huo, kutokana na hofu ya kuzuka mapambano makali kutoka kwa Wapalestina.

. Utawala huo ghasibu umefungua milango ya msikiti huo alfajiri ya leo kuwaruhusu watu wenye umri wa miaka 50 na kuendelea waweze kusali sala ya Asubuhi msikitini hapo. Hali ya hatari inashuhudiwa katika mji wa Quds kabla ya sala ya Ijumaa baada ya Harakati ya Fat’h kutangaza leo kuwa siku ya hasira dhidi ya maghasibu wa Kizayuni. Wito huo umetolewa kulaani hatua ya utawala huo ya kuuvunjia heshima msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu kama vile ambavyo Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS nayo kwa upande wake imeitisha maandamano makubwa kuutetea msikiti huo.../mh

1465757

captcha