IQNA

Mpango wa kuzuia ujenzi wa misikiti Ujerumani

15:36 - May 26, 2016
Habari ID: 3470338
Katika kuendelea chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya, chama kimoja cha kisiasa Ujerumani kimependekeza kuzuiwa ujenzi wa misikiti nchini humo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, chama cha misimamo mikali na cha mrengo wa kulia Ujerumani kijulikanacho kama The Alternative for Germany (AfD) kimependekeza usitishwaji ujenzi wa misikiti nchini humo.
Chama hicho, ambacho ni cha tatu kwa umashuhuri Ujerumani, hivi karibuni kilisema kitapinga kujenzi wa msikiti wa kwanza katika jimbo la Thuringia, mashariki mwa nchi hiyo.
Kiongozi wa chama hicho, Björn Höcke, amedai kuwa ujenzi wa msikiti katika jimbo hilo ni seehemu ya mpango wa muda mrefu wa Waislamu kueneza ushawishi wao. Chama hicho kimeitisha maandamano ya kupinga ujenzi wa msikiti huo.
Msimamo wa chama hicho ni jambo ambalo limeibua wasi wasi kuhusu kuibuka upya vyama vya mrengo wa kulia vyenye misimamo mikali ambavyo vinalengo kuibua malumbano na Waislamu tarkibani milioni nn wa Ujerumani. Chama cha AfD hivi karibuni kilizindua kampeni ya kusema 'Uislamu si Sehemu ya Ujerumani.
Chuo Kikuu cha Al Azhar kupitia taasisi yake ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu imetoa taarifa na kutoa wito kwa taasisi za Kiislamu Ujerumani kutumia uwezo wao wote wa kisheria kukabiliana na chuki zinazoenezwa na AfD.
Ikumbukwe kuwa chama cha AfD, ambacho kinapinga sera ya serikali ya nchi hiyo kuwakaribisha wakimbizi, kilitoa pigo kwa chama cha Kansela Angela Merkel katika uchaguzi w akieneo mwezi Machi.
Waislamu katika nchi za Magharibi wanakabiliana na wimbi jipya la chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia hata baada ya kuwa wamelaani vikali hujuma ya kigaidi duniani na hasa katika miji ya Ulaya ya Paris na Brussels.
3501032


captcha