IQNA

Tamasha la Chakula Halal nchini Canada

12:14 - July 18, 2017
Habari ID: 3471073
TEHRAN (IQNA)-Tamasha la Chakula Halal mjini Toronto, Canada, ni tamasha kubwa zaidi la chakula Halal eneo la Amerika Kaskazini na mwaka huu limewavutia Waislamu wengi waliojivunia mafanikio yao katika jamii.

Tamasha la 15 la Kila Mwaka la Chakula Halal Toronto 2017, limefanyika kwa muda wa siku mbili, Julai 15-16 katika Kituo cha Kimataifa cha Mississauga na kuwavutia wageni 35,000.

Wageni katika tamasha hilo wamepata fursa ya kutembelea vibana zaidi ya 200 vya vyakulla vilivyotayarishwa na migahawa bora zaidi ya halal mjini Toronto, bakery za mikate na keki na watengeneza bidhaa za vyakula.

"Waislamu wanazidi kuongezeka Canada na kwa msingi huo sekta ya vyakula Halal inazidi kuimarika,” amesema Salima Jivraj, mwasisi wa Tamasha la Chakula Halal. Ameongeza kuwa bada kuna nafasi ya kustawisha sekta hiyo huku akisisitiza umuhimu wa jamii kuelimishwa kuhusu chakula halali na tafauti baina ya chakula halali na kisicho halali.

Amesema kutoa elimu kwa jamii ni moja ya malengo ya tamasha hilo ambalo pia limeonyesha historia ya Waislamu Canada.

Hassam Munir aliyekuwa na kibanda cha Historia ya Waislamu Canada ameangazia historia ya miaka 200 ya Waislamu nchini humo. Anasema miongo kadhaa iliyoipita Waislamu wengi nchini humo hawakua wanajua kutafautisha baina ya vyakula halali na visivyo halali lakini sasa hali hiyo imebadilika.

Kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Nourish Food, sekta ya chakula Halal nchini Canada inakadiriwa kuwa yenye thamani ya dola bilioni moja na itazidi kustawi kwa idadi ya Waislamu nchini humo inatazamiwa kuongezeka kwa kasi. Waislamu nchini Canada wanakadiriwa kuwa milioni moja na nusu kati ya watu milioni 35.85 nchini humo.

3463390

captcha