IQNA

Msomi wa Malaysia

Misimamo mikali imetokana na Uwahabbi unaoenezwa na Saudia

16:04 - August 30, 2017
Habari ID: 3471149
TEHRAN (IQNA)-Msomi mmoja nchini Malaysia amesema kuwa tafsiri potovu za Uislamu zimevuruga uthabiti katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia na kuongeza kuwa, chanzo cha tatizo hilo ni walimu waliosoma Uwahabbi unaonezwa na Saudi Arabia.

Profesa Ahmad Fauzi Abdul Hamid, mwanasayansi wa siasa katika Chuo Kikuu cha Sains Malaysia ametoa kauli hiyo na kuongeza kuwa, katika muongo wa 1990, Uwahhabi ulienea sana na hivyo kupelekea kuibuka misimamo mikali inayoshuhudiwa sasa katika shule za nchi hiyo.

Ameongeza kuwa, waliosoma Uwahabbi katika kipindi hicho ndio sasa wanaoeneza misimamo mikali kote Malaysia. Profesa Fazui ametoa kauli hiyo katika warsha ya 'Uislamu Malaysia' iliyofanyika Jumanne katika Chuo Kikuu cha Sunway nchini humo.

Aidha amesema kuwa vyombo vya mahakama Malaysia vimeathiriwa vibaya na Uwahhabi kwani baadhi ya wanaohudumu katika mahakama hizo walijazwa fikra za Uwahhabi wakiwa shuleni na katika vyuo vikuu.

"Kuna majaji ambao walisoma itikadi za Uwahhabi katika vyuo vikuu kama vile Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Malaysia (IIUM), na ni kwa sababu hiyo ndio tunaona wakitoa hukumu zenye misimamo mikali ya kidini."

Msomi huyo wa Malaysia amesema Waarabu waliokuja na Uislamu katika karne za awali nchini Malaysia walifanikiwa kwa sababu hawakuonyesha uhasama kwa utamaduni wa nchi hiyo. Hatahivyo amesema wahubiri wanaokuja nchini humo hivi sasa kutoka nchi za Kiarabu wana misimamo mikali na finyu ambayo haistahamili utamaduni wa Malaysia.

3463795


captcha