Uchunguzi huo umebaini iwapo mfungwa ni Muislamu au mwenye asili ya Afrika basi kuna uwezekano wa asilimia 40 kuwa atakandamizwa na kudhulumiwa ikilinganishwa na wafungwa wazungu.
Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa asilimia 29 ya wafungwa Waislamu hawapati fursa ya kazi zenye pato au fursa za kusoma wakiwa gerezani katika hali ambayo kiwango hicho ni asilimia 17 kwa wafungwa Wakristo. Katika magereza ya Uingereza wafungwa hufanya kazi ambazo huwasaidia kupata pato wakiwa wanatumikia vifungo vyao .
Idadi ya wagunwa Waislamu Uingereza inaripotiwa kuongoezeka maradufu tokea mwaka 2002 huku wakiendelea kudhulumiwa pasina kuwepo taasisi za kuwatetea.