IQNA

Bunge la Iran laidhinisha muswada wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel

19:48 - May 12, 2020
Habari ID: 3472759
TEHRAN (IQNA) - Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) imepasisha kwa kauli moja muswada wa dharura wa kukabiliana na njama na uhasama za utawala wa Kizayuni wa Israel, dhidi ya amani na usalama wa kieneo na kimataifa.

Muswada huo umepasishwa kwa kura 43 za 'Ndio' na 0 ya 'Hapana' katika kikao kilichofanyika mapema leo Jumanne cha Bunge hilo.

Anga ya bunge hilo ilihinikiza kwa nara za "Mauti kwa Israel" zilizokuwa zikitolewa na wabunge wa Jamhuri ya Kiislamu wakati wa kikao hicho.

Mojtaba Zonnour, Mwenyekiti wa Tume ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ya Bunge la Iran amesema muswada huo uliopasishwa una vipengee 14 vilivyoainisha hatua za kuchukuliwa na nchi hii, dhidi ya mienendo ya kuvuruga amani ya utawala haramu wa Israel.

Amesema utawala huo bandia unalitumia vibaya janga la COVID-19, kuhujumu maslahi ya kitaifa na kimataifa ya Iran ya Kiislamu. Hata hivyo amesisitiza kuwa njama hizo za utawala wa Kizayuni wa Israel zitagonga mwamba.

Baada ya kupasishwa muswada huo, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Ali Larijani ameitaka kamati husika kuutathmini haraka iwezekanavyo, ili uwekwe kwenye ajenda ya wiki ijayo ya bunge hilo.

3898357

captcha