Akizungumza mjini Tehran Jumanne wakati wa kufunga Tamasha la 36 la Qur'ani na Itrat katika Wizara ya Sayansi, Utafiti naTeknolojia, Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Sidiqquie amesema tokea kuteremshwa kwake, Qur'ani Tukufu imetoa changamoto kwa wengine kuwasilisha sura kama zake na hakuna aliyeweza kufanya hivyo.
Amesema ni miujiza michache tu ya Qur'ani iliyoweza kugunduulika hadi sasa na kwamba badi kuna nukta nyingi sana za siri za Qur'ani ambazo bado mwanadamu hajaweza kuzibaini.
Amesema Qur'ani Tukufu ina maelezo ya kisayansi kama vile kuhsu embryolojia, mime n.k ambayo wanadamu walikuwa hawayajui wakati wa kuteremshwa kwake.
Hujjatul Islam Siddiquie ameashiria aya ya pili ya Sura al Baqara isemayo:" Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu." Na kuongeza kuwa, Qur'ani Tukufu ni kitabu cha kumuongoza mwanadamu ili aweze kufukia ukamilifu.