IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Marekani na Uingereza zinaunga mkono hujuma ya Israel Ghaza

7:53 - July 13, 2014
Habari ID: 1428809
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema Marekani na Uingereza zinaunga mkono hujuma inayoendelea ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.

Akizungumza Jumamosi usiku mjini Tehran, Kiongozi Muadhamu amesema nchi hizo mbili si tu kuwa hazijali kuhusu hujuma za Israel huko Ghaza bali pia zinaunga mkono rasmi hujuma hizo ambazo zimepelekea Wapalestina zaidi ya 150 kupoteza maisha, aghalabu yao wakiwa ni wanawake na watoto wasio na hatia na wanaodhulimuwa. Kiongozi Muadhamu pia amesema katika dunia ya leo, madola makubwa ya kibeberu yanaunga mkono kila aina ya uovu na ufisadi maadamu ni kwa maslahi yao na mkabala wa hilo madola hayo yanapinga na kukabiliana kinyama na kikatili na kila utakasifu na utukufu ambao unaenda kinyume na maslahi yao. Ayatullah Khamenei ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika mkesha wa kukumbuka siku ya kuzaliwa Mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hassan Mujtaba AS. Kikao hicho kilihudhuriwa na kundi la wahadhiri wa lugha na fasihi ya kifarsi, malenga wakongwe na vijana hapa Iran pamoja na kundi la malenga wanaozungumza lugha ya Kifarsi kutoka Afghanistan, Tajikistan, Pakistan na India. Akihutubu katika kikao hicho, Kiongozi Muadhamu sambamba na kutoa salamu za pongezi kwa mnasaba huo mtukufu ameashiria hali ya kusikitisha katika dunia ya leo ni kuhoji, je, kwa kuzingatia kuwa malenga wana  uwezo wa kudiriki, kufahamu wana majukumu gani ya kutekeleza kuhusu matukio na hali ya sasa duniani? Katika kujibu swali hilo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kutokana na uwezo walio nao, malenga wanapaswa kuwasaidia wanaodhulumiwa sambamba na kubainisha haki na ukweli kupitia mashairi yao. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amewanasihi Waislamu kutumia fursa inayojitokeza katika nyusiku za Laylatul Qadr katika Mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

1428823

captcha