IQNA

Baraza la Usalama lataka kusimamishwa vita Ghaza

21:39 - July 22, 2014
Habari ID: 1432292
Hatimaye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Julai 20 lilivunja kimya chake na kudai kuwa linasikitishwa na idadi kubwa ya raia wanaouliwa na kujeruhiwa huko Ukanda wa Ghaza na kutaka kusimamishwa mara moja kile ilichokitaja kuwa ni uhasama.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatoa matamshi hayo katika hali ambayo ni utawala wa Kizayuni ndio ulioanzisha na ungali unaendeleza mashambulio yake ya kikatili dhidi ya raia wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza wasio na hatia yoyote. Eugene Gasana Balozi wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa, ambaye nchi yake inashikilia uwenyekiti wa kiduru wa Baraza la Usalama amesema kuwa, nchi wanachama wa baraza hilo zimebainisha wasiwasi wao mkubwa kutokana na kuongezeka idadi ya raia wanaouawa na kujeruhiwa huko Ghaza.

Wakati huo huo Riyad Mansour Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema amekatishwa tamaa na taarifa iliyotolewa na Baraza la Usalama la umoja huo akisema kuwa wao walitaraji kwamba baraza hilo lingewasilisha azimio la kulaani ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina.

1431813

captcha