IQNA

Mashindano ya Qur’ani yanalenga kuhuisha umoja wa Waislamu

20:50 - January 01, 2015
Habari ID: 2666237
Mwenyekiti wa Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran amesema lengo la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu ni kuimarisha itikadi za wanafunzi wa vyuo vikuu katika ulimwengu wa Kiislamu ili kuhuisha umoja wa Waislamu kueneza ustaarabu mpya wa Kiislamu.

Hamid Ridha Twaibi ameyasema hayo leo alasiri mjiini Tehran alipohutubu katika ufunguzi wa Mashindano ya Tano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu. Akizungumza katika kikao hicho cha ufunguzi, ambacho pia kilihudhuriwa na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, aliwakaribisha kwa moyo mkunjufu washiriki kutoka nchi za kigeni waliofika katika duru hii ya mashindano. Amebainisha furaha yake kubwa kutokana na Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu imeandaa mashindano haya kwa mnasaba wa Wiki ya Umoja wa Kiislamu.
Hamid Ridha Twaibi amebainisha kuwa baadhi ya makundi yanasababisha kudidimia ustaarabu wa Kiislamu kutokana na matendo yao maovu. Ameongeza kuwa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu yanalenga kuhuisha tena umoja wa Kiisalmu duniani. Mkuu huyo wa Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu amesema mashindano Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu hufanyika kila miaka miwili nchini Iran na kwamba yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2006 mjini Isfahan kwa kuwaleta pamoja washiriki kutoka nchi 29. Duru a pili ilifanyika Tehran ambapo kulikuwa na washiriki kutoka nchi 40 duniani huku duru ya tatu ikifanyika Mashhad na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi 41. Duru ya nne ya mazungumzo hayo ilifanyika katika mji wa Tabriz na kuwashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka nchi 50. Amebainisha kuwa Mashindano ya Tano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu yaliyofunguliwa leo Alkhamisi katika ukumbi wa Mnara wa Milad  katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran yana washiriki 66 kutoka nchi 47 . Washiriki hao ambao ni  ni wanafunzi wa vyuo vikuu na watashindana kwa muda wa siku nne kusoma (qiraa) na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.../mh

2664192

captcha