IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya wanafunzi wa shule kufanyika Iran

21:22 - August 04, 2016
Habari ID: 3470493
Duru ya tano ya mashindano ya kimatiafa ya Qur’ani ya wanafunzi wa shule yatafanyika nchini Iran mwezi Februari mwaka 2017.

Mohammad Ridha Purmoin, ambaye ni msimamizi wa mashindano hayo, amemwmabia mwandishi wa IQNA kuwa nchi 40 tayari zimeshathibitisha kushiriki katika mashindano hayo ya Qur’ani.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yatafanyika katika kategoria mbili za kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu ambapo kutakuwa na vitengo tafauti vya wasichana na wavulana.

Purmoin amebaini kuwa mashindano hayo ambayo yatafanyika mjini Tehran yanalenga kuhimjiza wanafuynzi shuleni kujihusisha zaidi katika harakati za Qur’ani sambamba na kuandaa mazingira maridhawa ya wanafunzi wa shule kushindana katika ustadi wa usomaji Qur’ani.

Halikadhalika amesema lengo jingine muhimu la mashindano hayo ni kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu.

Mashindano hayo yalifanyika mara nne kwa mara ya kwanza katika miaka ya awali ya muongo wa tisini na sasa ni takribani miongo miwili tokea mashindano hayo yasimamishwe kwa kwa sababu mbali mbali.

Mashindano hayo ya Qur’ani yameandaliwa na Wizara ya Elimu ya Iran.

3519762

captcha