IQNA

Utawala dhalimu wa Israel wabomoa msikiti Ukingo wa Magharibi

19:31 - November 05, 2021
Habari ID: 3474520
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamebomoa msikiti wa Wapalestina katika mji wa Duma, kusini mwa eneo linalokaliwa kwa mabavu na utawala huo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa katika jinai hiyo ya siku ya Alhamisi, buldoza za jeshi la utawala wa kikoloni wa Israel zilibomoa msikiti ambao umekuwa ukitumiwa kwa muda wa miaka miwili na Wapalestina katika eneo hilo.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini katika Mamlaka ya Ndani ya Palestina imelaani vikali jinai hiyo ya Israel na kusema ni ukiukwaji wa wazi wa matukufu ya Waislamu.

Hivi karibuni Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, hakuna dola lolote duniani lenye uwezo wa kulilazisha taifa la Palesitna liondoke katika ardhi zake na kuzifumbia macho.

Ismail Hania alisema pia kuwa, makundi ya muqawama yamewatangazia wakazi wa eneo la Ukingo wa Magharibi na hasa Sheikh Jarrah huko Quds (Jerusalem) kwamba wanapaswa kusimama imara kulinda haki na ardhi yao.

Katika kipindi cha karibuni, Wazayuni maghasibu wamekuwa wakifanya njama kubwa za kuwalazimisha Wapalestina waondoke kwenye maeneo yao kwa kubomoa makazi yao na msikiti.

3476341/

captcha