IQNA

OIC yamteua mjumbe maalum wa Afrika

22:40 - March 26, 2022
Habari ID: 3475078
TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imethibitisha uteuzi wa mjumbe maalum wa Afrika.

Katika mkutano wa tarehe 22 - 23 Machi katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC lilipitisha azimio la umoja huo kumteua Nassirou Bako Arifari kama Mjumbe Maalum, ilisema taarifa ya jumuiya hiyo ya mataifa 57 ya Waislamu katika taarifa Alhamisi.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Benin, Afrika Magharibi, Arifari pia amefundisha katika vyuo vikuu mbalimbali, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

"Uamuzi huu unasukumwa na imani ya Baraza juu ya umuhimu wa bara la Afrika na masuala yake kwani idadi kubwa ya nchi wanachama wa OIC wanatoka bara la Afrika," ilisema taarifa hiyo.

"Uamuzi huo pia ni kujibu matakwa ya Mkutano wa (2019) wa Makkah Al-Mukarramah ya kutaka uangalizi zaidi kutolewa na OIC kwa Afrika na masuala ya Afrika."

Mawaziri hao walikusanyika mjini Islamabad siku ya Jumanne kwa ajili ya mkutano chini ya mada "Kushirikiana kwa Umoja, Haki na Maendeleo."

3478272

Kishikizo: oic afrika waislamu
captcha