Msichana huyo kwa jina Jani Adham Naeem Ashur, ana umri wa miaka 13, na anatoka Ukanda wa Gaza.
Hafla ilifanyika hivi karibuni ambapo alienziwa na maafisa wa Qur'ani wa eneo hilo kwa mafanikio yake makubwa.
Hafla hiyo iliandaliwa na taasisi ya kutoa misaada ya Qur'ani ya Iqra, ambayo rais wake alibainisha matarjio yake kwamba binti huyu aliyehifadhi Qur'ani atautumikia Uislamu na Qur'ani Tukufu.
Habari za kufanikiwa kwa Jani zimeenea kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu hazijawahi kutokea. Hakuna mtu mwingine anayejulikana kuwa aliweza kuhifadhi Qur'ani yote ndani ya mwezi mmoja tu.
Qur'ani Tukufu ndio Maandiko pekee ya kidini ambayo yanaweza kuhifadhiwa kikamilifu na wafuasi wake.
Watu wasiohesabika katika kila umma wa Kiislamu wamehifadhi Qur'an tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa.
Quran ina Juzuu (sehemu) 30, Sura (sura) 114 na aya 6,236, kwa hivyo kuhifadhi Kitabu kitakatifu kizima si kazi rahisi.
3480125