IQNA

u

Shule ya mtandaoni ya Qur'ani yazinduliwa kwa ajili ya Waalgeria

19:24 - August 22, 2022
Habari ID: 3475664
TEHRAN (IQNA)- Shule ya mtandaoni ya kufundisha Qur'ani Tukufu na lugha ya Kiarabu kwa raia wa Algeria wanaoishi katika nchi mbalimbali za dunia ilizinduliwa kwa idhini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hii.

Hourieh Sohaili mkurugenzi wa "Dar Al-Jazair (Nyumba ya Algeria)" nchini Uhispania amesema: "Shule hii ilizinduliwa kwa lengo la kutoa mafunzo haya muhimu kwa watu wa  Algeria wanaoishi nje ya nchi.

Ameongeza kuwa: “Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria imekubaliana na mpango huu na imetangaza utayari wake wa kuuunga mkono kwa ushirikiano wa idara maalumu hususan Wizara ya Elimu”.

Mradi huu unalenga kuhifadhi mila,desturi na maadili ya taifa la Algeria, ambalo asili yake ni Uislamu, na pia kutoa mafunzo ya Qur’ani na lugha ya Kiarabu, ili vizazi vipya vijue utambulisho wao na kuuhifadhi kutoka kwa aina mbalimbali za kutengwa na kutoweka.

Mpango huu pia unawawezesha Waalgeria kuwa popote pale duniani kwa kunufaika na programu zinazotayarishwa na makundi maalumu, kufaidika na elimu ya dini ya Kiislamu na lugha ya Kiarabu, na kutimiza matakwa ya wazazi wanaosisitiza kuufundisha watoto wao Uislamu na Qur'ani.

Mpango huu pia unalenga kuimarisha moyo wa uzalendo miongoni mwa Waalgeria wanaoishi nje ya nchi na umezingatia watu ambao hawana njia za kujifundisha Qur'ani au shule za Kiislamu na misikiti haipatikani katika maeneo yao ya kuishi.

4079961

captcha