Zaidi ya wavulana na wasichana 10,000 wanaosoma katika shule mbali mbali walishiriki katika mashindano hayo.
Mashindano hayo yameandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Wakfu ya nchi hiyo na Wizara ya Masuala ya Kidini na Elimu.
Walishindana katika kategoria ya usomaji wa Qur'ani Tukufu huku wakizingatia kanuni za Tajweed, Sawt na Lahn.
Wataalamu kadhaa kutoka Wizara ya Wakfu na masuala ya kidini walihudumu kama wajumbe wa jopo la waamuzi wa mashindano hayo.
Shughuli za Qur'ani ni za kawaida sana huko Palestina, katika Ukanda wa Gaza na katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, huku programu za usomaji na kuhifadhi Qur'ani zikifanyika kwa mwaka mzima bila kusitishwa.
4108183