IQNA

Kimbunga cha Al Aqsa

Mhimili wa Muqawama hautaruhusu Wazayuni watekeleza Nakba nyingine Palestina

16:42 - October 30, 2023
Habari ID: 3477811
TEHRAN (IQNA) - Mhimili wa muqawama (mapambano ya Kiislamu) uko macho na hautaruhusu utawala wa Kizayuni kuibua Nakba (maafa) tena dhidi ya ya watu wa Palestina, mchambuzi wa kisiasa wa Lebanon alisema.

Talal al-Atrisi ambaye ni profesa wa sosholojia ameyasema hayo katika mahojiano na IQNA ambapo amezungumzia majaribio ya utawala wa Kizayuni kurejesha sura yake iliyosambaratika kufuatia Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoanzishwa na harakati ya muqawama ya Hamas tarehe 7 Oktoba.

Amesema mauaji yanayotekelzwa na utawala dhalimu wa Israel dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza, ambayo yanajumuisha hata mashambulizi ya mabomu katika hospitali ambazo zimejaa waliojeruhiwa katika mashambulizi hayo au wanaopata hifadhi, ni dalili ya kukata tamaa kwa utawala huo.

Utawala ghasibu wa Israel unajaribu kulipiza kisasi kutoka kwa Hamas na kurejesha sura yake ya bandia ya kutoshindwa ambayo ilipata pigo kubwa katika operesheni ya Oktoba 7, alisema.

Leo, uwezo wa kuzuia jeshi la Israel umeharibiwa na taswira yake ya kutoshindwa ilivunjwa, alisema.

Wakati Wazayuni wakiendelea kusema kwamba uvamizi wa ardhini unakaribia, hawajaonyesha mwelekeo wowote wa kufanya mashambulizi kama hayo, alibainisha.

Atrisi ameongeza kuwa moja ya malengo ya mashambulizi ya kinyama ya Gaza ni kudhoofisha umaarufu wa Hamas.

Alisema adui pia analenga kuwalazimisha Wapalestina wanaoishi Gaza kuondoka katika eneo hilo na kwenda kukaa katika maeneo mengine kama vile Sinai nchini Misri.

Kuhamishwa kwa vikosi vya watu wa Gaza ni hali ambayo maafisa wa kisiasa na kijeshi wa Wazayuni wanafuatilia kupitia mashambulizi ya anga, mchambuzi huyo alisema.

Watu wa Palestina na mhimili wa muqawama hata hivyo, hawataruhusu Nakba nyingine itekelezwe na Kizayuni, alisisitiza.

Nakba ambayo pia unajulikana kwa jina la Janga la Palestina, ilijiri mwaka wa 1948 kwa kuhamishwa Wapalestina walio wengi na utawala wa Kizayuni.

Atrisi amesema Wapalestina wako macho zaidi na wanazingatia zaidi matukio ya leo na hawatakubali Nakba mpya, hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba mapambano hayo ni ya kutumia silaha na macho.

Aliendelea kusema kuwa, watu wa Palestina, wawe ni wale wa Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan au kwingineko, wana motisha kubwa ya kukabiliana na utawala unaokaliwa kwa mabavu.

Inafaa kuashiria hapa kuwa katika kukabiliana na jinai za Wazayuni, vikosi vya muqawama vya Palestina vilianza operesheni ya "Tufani ya Al Aqsa" ukanda wa Ghaza dhidi ya ngome za utawala wa Kizayuni  wa Israel kuanzia Jumamosi, Oktoba 7, 2023.

Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, jeshi la Kizayuni, ambalo halina uwezo wa kukabiliana na wapiganaji wa muqawama, limekuwa likishambulia kwa mabomu maeneo ya raia, hospitali, vituo vya kidini na shule huko Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Afya ya Palestina, zaidi ya Wapalestina 8000 wameuawa shahidi na wengine takriban 20,000 wamejeruhiwa tangua kunza jinai mpya ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika ukanda wa Ghaza. Aghalabu ya waliopoteza maishani wanawake na watoto.

4177758

Habari zinazohusiana
captcha