Programu hiyo imeandaliwa kwa wagombea na wajumbe wa jopo la majaji.
Tehran ni mwenyeji wa Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran kwa kushirikisha wahifadhi na wasomaji 99 kutoka nchi 44.
Sambamba na hayo, Awamu ya 8 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi wa Shule inaendelea katika mji mkuu wa Iran.
Washiriki wa hafla zote mbili za Qur'ani Tukufu na wajumbe wa jopo la majaji au waamuzi walifanya ziara katika kaburi la Imam Khomeini (RA), marehemu muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, huko Rey,kusini mwa Tehran, siku ya Ijumaa.
Kama mpango mwingine wa kando, wametembelea Bustani ya Makumbusho Kujihami Kukatifu siku ya Jumamosi na Husseiniyah Jamaran , nyumba ya hayati Imam Khomeini (RA) kaskazini mwa Tehran siku ya Jumapili.
Siku ya Jumatatu, wamepangwa kutembelea Mnara wa Milad, mnara mrefu zaidi nchini Iran.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni hafla ya kila mwaka ambayo huwavutia wasomaji na wahifadhi Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
4200097