IQNA

­­­­­­­­­Ahadi ya Kweli

Iran yaonya itatoa jibu kali iwapo utawala wa Israel utafanya harakati yoyote ya kifidhuli

19:54 - April 14, 2024
Habari ID: 3478685
IQNA-Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utafanya harakati yoyote ya kifidhuli utakabiliwa na jibu madhubuti, zito na kali zaidi.

Kufuatia jibu lililotolewa mapema leo na vikosi vya ulinzi vya Iran kwa hujuma ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria, Seyyed Ebrahim Raisi, Rais wa Iran ameashiria operesheni hiyo ya kihistoria, ya nguvu na ushindi iliyotekelezwa na vikosi vya ulinzi vya Iran na akasema, vijana mashujaa na wenye ghera wa taifa la Iran katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), kwa mashauriano na ushirikiano na sekta zote za ulinzi na kisiasa, wamefungua ukurasa mpya katika historia ya nguvu na uwezo wa Iran na kutoa somo lenye mazingatio kwa adui Mzayuni.

 

Raisi amesema, kumtia adabu mchokozi ambayo ni ahadi ya kweli aliyotoa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imetimizwa; na vikosi vya ulinzi vya kujivunia vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa nguvu na uwezo kamili vimelenga kupitia operesheni za mchanganyiko maeneo na vituo vya kijeshi vya utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu; na hatua hiyo imechukuliwa kwa kutumia haki halisi iliyonayo Iran ya kujihami kisheria.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, ujumbe uliotolewa na shambulio la makombora na ndege zisizo na rubani lililofanywa usiku wa kuamkia leo Jumapili na Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni, kwa upande wa umma wa Kiislamu ni kuthibitisha nguvu na uwezo na kuzuia hujuma. Ameongeza kuwa, kwa upande wa adui ni kumtia hofu na kumdhalilisha na akasema: katika miezi sita iliyopita na hasa katika siku 10 za hivi karibuni, Iran imetumia kila nyenzo na suhula kikanda na kimataifa ili kuizindua jamii ya kimataifa juu ya hatari kubwa ya kutochukuliwa hatua na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya ukanyagaji wa sheria wa mtawalia unaofanywa na utawala wa Kizayuni, lakini kwa masikitiko, Baraza la Usalama liko chini ya satua na ushawishi wa Marekani na baadhi ya waungaji mkono wengine wa utawala bandia wa Israel, na hivyo limeshindwa kutekeleza majukumu yake.

 

Aidha Raisi amesema, "Muqawama" ni msamiati mkuu wa kuhuisha amani na usalama katika eneo na kupinga uvamizi na kila aina ya ugaidi na akasisitiza kwamba kwa mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran chimbuko la mgogoro katika eneo ni mauaji ya kimbari na khulka ya ukatili ya utawala wa Kizayuni.

 Naye Meja Jenerali Mohammad Baqeri, Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Iran, ametangaza kwamba mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu yamekamilika (Israel), na kuonya juu ya majibu "nguvu zaidi" ikiwa utawala wa Israel utajibu mashambulizi hayo.

Baqei alisema kuwa operesheni hiyo ni adhabu kwa utawala huo, akibainisha kuwa ililenga tu maeneo ya kijeshi na uwezo ambao ulikuwa na jukumu la kuanzisha mashambulizi ya Aprili 1 dhidi ya jengo la ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus.

"Operesheni hii imetekelezwa kwa sababu utawala wa Kizayuni wa Israel umevuka mstari mwekundu wa [Iran] na jambo hilo haliwezi kuvumiliwa kwa njia yoyote," alisisitiza.

"Tulikuwa na uwezo wa kurusha mara kumi zaidi ya makombora na ndege zisizo na rubani lakini hatukufanya hivyo na tulijaribu kutekeleza adhabu yenye kikomo," kamanda mkuu aliongeza.

 

captcha