Katika taarifa siku ya Ijumaa, Amnesty imesema jeshi la
Nigeria liliua zaidi ya Waislamu 350 wanachama wa Harakati ya Kiislamu Nigeria
inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky. Ripoti hiyo imefichua kuwa, jeshi la
Nigeria lilijaribu kuficha ushahidi wa jinai hiyo kwa kuwazika waathrika katika
makaburi ya umati huku watu wa kawaida wakizuia kufika katika baadhi ya maeneo
ya jinai hiyo katika mji wa Zaria jimboni Kaduna.
Ikumbukwe kuwa Desemba 12 mwaka jana, wanajeshi wa Nigeria waliwashambulia
Waislamu waliokuwa katika kituo cha Kiislamu Zaria na kuwatuhumu kuwa walifunga
njia ya msafara wa mkuu wa jeshi kwa njama ya kumuua.
Waislamu wa eneo hilo wamepinga vikali tuhuma hizo. Siku moja baadaye, jeshi la
Nigeria lilivamia nyuma ya Sheikh Zakzaky na kumtia mbaroni sambamba na kuua
mamia ya Waislamu waliokuwa wakimlinda. Katika matukio hayo mawili, mamia ya
wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria waliuawa kwa umati, wakiwemo watoto
wawili wa Sheikh Zakzaky. Baadhi ya duru zinadikeza kuwa waliouawa katika tukio
hilo ni Zaidi ya elfu moja. Amnesty International imesema Jeshi la Nigeria
jeshi la Nigeria liliwachoma moto Waislamu hai sambamba na kuteketeza nyumba na
kutuma miiili katika makaburi ya umati. Ripoti hiyo imesema sit u kuwa jeshi la
Nigeria lilitumia nguvu ziada dhidi ya wanawake, watoto na wanaume na kisha
kuwaua kwa umati, bali pia kumefanyika njama za makusudi za kufika ukweli
kuhusu jinai hiyo. Aidha Amnesty imeutaka utawala wa Rais Muhammadu Buhari
kuchunguza muaji hayo ya Waislamu wasio na hatia.