IQNA

Ripoti: Jeshi la Nigeria liliwaua na kuwazika Waislamu 348 Zaria

9:47 - August 03, 2016
Habari ID: 3470492
Jopo la uchunguzi kuhusu mauaji ya Waislamu kaskazini mwa Nigeria limekiri kuwa jeshi la nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika liliuawa Waislamu 348 katika mji wa Zaria jimbo la Kaduna.

Jopo hilo limethibitisha uchunguzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lililosema kuwa Waislamu karibu 350 wa madhehebu ya Shia waliuwa na askari wa Nigeria katika mji wa Zaria. Jopo hilo la majaji limependekeza kufunguliwa mashtaka wanajeshi waliouhusika na mauaji hayo ya kikatili mwishoni mwa mwaka jana.

Mwezi Aprili mwaka huu, Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International lilitangaza kuwa, jeshi la Nigeria liliua zaidi ya Waislamu 350 wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky mwezi Disemba mwaka jana.

Itakumbukwa kuwa tarehe 14 Disemba mwaka jana 2015, siku moja baada ya jeshi la Nigeria kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya Waislamu katika mji wa ZariaIkumbukwe kuwa kati ya Desemba 12-14 mwaka 2015, Jeshi la Nigeria liliwashambulia wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria IMN katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi lilidai kuwa wafuasi wa IMN walikuwa na jama ya kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo. Jeshi hilo katili liliizika miili ya waliouawa katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo.

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria hata hivyo inasisitiza kuwa zaidi ya Waislamu 1000 waliuliwa na jeshi la nchi hiyo katika hujuma hiyo.

Aidha Jeshi la Nigeria lilimkamata Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria akiwa pamoja na mke wake. Hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky inaripotiwa kuwa mbaya huku taarifa zikisema amepoteza jicho moja mbali na majeraha mengine mwilini. Serikali ya Nigeria inamshikilia kiongozi huyo wa Kiislamu tokea Desemba mwaka jana pasina kumfungulia mashtaka.

3460572

captcha