Idara ya Masuala ya Haramein Sharifein nchini Saudia imetangaza kuwa tayari kumsaidia mvumbuzi huyo kutayarisha kazi yake hiyo kwa ajili ya kutumiwa na wenye ulemavu wa macho.
Kwa mujibu wa taarifa, mkuu wa Idara ya Masuala ya Haramein Sharifein ametangaza kuwa amekutana na mvumbuzi huyo, Mashaal Al Harsani kwa ajili ya kujadili kuhusu Qur’ani hiyo ya kidijitali ya lugha ya Braille na namna itakavyoundwa na hatimaye kuwafikia wenye ulemavu wa macho.
Amesema lengo la kutayarishwa Qur’ani ya kidijitali kwa lugha ya Braille ni kuwahimiza wenye ulemavu wa macho kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Alfabeti ya Braille, huwasaidia watu wasioona au wenye ulemavu wa macho kusoma. Braille husomwa na wenye ulemavu wa macho kwa kupitisha vidole juu ya karatasi.