IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washiriki 500 waliohifadhi Qur'ani washiriki Mashindano ya Dubai

11:30 - October 17, 2022
Habari ID: 3475941
TEHRAN (IQNA) – Zaidi ya washiriki 500 waliohifadhi Qur’ani Tukufu wameshiriki katika mashindano ya kila mwaka ya Qur’ani yanayoandaliwa na Vituo vya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu vya Maktoum huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Idara ya Masuala ya Kiislamu na Shughuli za mji huo (IACAD) ilisema awamu ya mwisho ya toleo la 2022 imeanza kwa kushirikisha wanaume 172 na wanawake 339.

Kwa mujibu wa Hamad Muhammad al-Khazraji, mkurugenzi wa Vituo vya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu vya Maktoum, usajili wa mashindano hayo ulifanyika mwezi Agosti kupitia tovuti ya IACAD.

Alisema makundi ya tukio hilo ni pamoja na kuhifadhi Quran nzima kwa rika zote, kuhifadhi Juzu (sehemu) 20 za Qur'ani kwa rika zote, kuhifadhi juzuu15, 10, 5, na 3 kwa wale waliozaliwa baada ya 2011. Kuhifadhi Juzuu 30 kwa wale waliozaliwa baada ya 2014, na kusoma Juzuu 5 za mwisho za Kitabu Kitakatifu.

Khazraji alibainisha kuwa kategoria ya mwisho ni ya raia wa UAE waliozaliwa mwaka wa 1969 na mapema zaidi.

Washindi watatangazwa na kutunukiwa katika hafla iliyopangwa kufanyika katika wiki ya kwanza ya Novemba, aliendelea kusema.

Vituo vya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu vya Maktoum vinahusishwa na Idara ya Masuala ya Kiislamu na Shughuli za Hisani ya Dubai, ambayo malengo yake, kwa mujibu wa tovuti yake, ni pamoja na kueneza na kukuza maadili ya Uislamu wenye msimamo wa wastani, kuendeleza kazi ya hisani na kujenga misikiti kwa mujibu wa kanuni kimataifa.

Vituo hivyo huandaa kozi za Qur'ani, zikiwemo za Kuhifadhi Qur'ani, kwa ajili ya wanafunzi wa kiume na wa kike bila malipo.

4092311

captcha