IQNA

Vikosi vya Israel vyahujumu Msikiti wa Al Aqsa, Quds

16:08 - July 26, 2015
Habari ID: 3335481
Vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimeuvamia Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu. Kufuatia hujuma hiyo ya mapema Jumapili asubuhi, kumeibuka mapigano baina ya polisi ya Israel na Waislamu waliokuwa ndani ya msikiti huo mtakatifu.

Wapalestina waliokuwa hapo walikabiliana na polisi hao wa Israel ili kuwazuia kuingia katika ukumbi mkuu wa msikiti huo. Utawala wa Kizayuni umesema askari wake kadhaa wamejruhiwa katika machafuko hayo huku Wapalestina sita wakitiwa mbaroni.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuwawekea vizingiti Wapalestina wanaoenda kuswali katika msikiti wa al Aqsa. Uchunguzi umebaini kuwa asilimia 90 ya Wapalestina wanaamini kuwa Israel inatekeleza njama za kubomoa Msikiti wa Al Aqsa na mahala pake kujenga hekalu la Kiyahudi.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unatekeleza njama za kuuyahudisha mji wa Quds kwa kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, kubomoa maeneo ya kihistoria na kwuatimua Wapalestina kutoka makaazi yao asili. Msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu na sehemu ya tatu takatifu katika Uislamu baada ya Masjid al-Haram mjini Makka and Masjid al-Nabawi mjini Madina.../mh

3335343

captcha