IQNA

Kikao cha dharura cha nchi za Kiislamu kuhusu Quds

17:43 - August 07, 2015
Habari ID: 3339755
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeitisha kikao cha dharura cha viongozi wa nchi za Kiislamu kujadili kadhia ya Quds na Msikiti wa Al Aqsa.

Kwa mujibu wa taarifa ya OIC, kikao hicho kinachotazamiwa kufanyika Morocco kimeitishwa na Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas kutokana na kuwa kadhia ya Palestina ina umuhimu wa kipekee katika OIC na katika umma mzima wa Waislamu.
Katika taarifa  OIC imesema: "Kikao cha viongozi wanachama ni katika fremu ya jitihada zisizo na kikomo za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kuunga mkono taifa na kadhia ya Palestina katika uga wa kieneo na kimataifa kwa lengo la kuhitimisa kukaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni ardhi za Palestina na kuundwa nchi huru ya Palestina mji wake mkuu ukiwa ni Quds Shariff." OIC imesema bado kunafanyika mashauriano na nchi wanachama kuhusu wakati muafaka wa kufanyika kikao hicho.Katika wiki za hivi karibuni kumeshuhudiwa kuongezka wimbi la hujuma ya  walowezi wa Kizayuni katika Msikiti wa Al Aqsa.
Lengo la utawala wa Kizayuni ni kuuharibu kabisa Msikiti wa Al Aqsa  na hatimaye kuliyahudisha eneo hilo. Jeshi la Utawala wa Israel limekuwa likiwapa himaya masetla wa Kizayuni wanaouhujumu Msikiti wa Al Aqsa. Eneo hilo ni la tatu kwa utakatifu katika Uislamu mbali na kuwa kibla cha kwanza cha Waislamu.../mh

3339686

captcha