IQNA

Wazayuni wenye misimamo mikali wauhujumu Msikiti wa Al Aqsa

13:40 - June 06, 2016
Habari ID: 3470363
Magenge ya walowezi wa Kizayuni wakiwa chini ya humaya ya askari wa utawala haramu wa Israel Jumpili wameuhujumu Msikiti wa Al Aqsa katika Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu.
Mkurugenzi wa Msikiti wa Al Aqsa, Sheikh Omar al-Kiswani amesema zaidi ya walowezi 200 waliuhujumu Msikiti wa Al Aqsa wakipitia mlango wa Maghariba cini ya ulinzi mkali wa askari wa utawala haramu wa Israel.
Al Kiswani ameukosoa vikali utawala haramu wa Israel kwa kutekekza uchokozi huo katika mkesha wa kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Wazayuni waliuvamia Msikiti wa Al Aqsa katika kukbukumbu ya kuvamia na kuukali kwa mabavu mji wa Quds Mashariki mwaka 1967.
Siku kama ya jana miaka 49 iliyopita inayosadifiana na tarehe 5 Juni 1967 vilianza vita vya tatu kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu na mataifa ya Kiarabu. Katika siku hiyo, vikosi vya anga vya utawala wa Israel vilishambulia majeshi ya nchi tatu za Misri, Syria na Jordan kwa muda wa masaa mawili baada ya kufanya operesheni ya kushtukiza kwa kuvuka mipaka ya nchi hizo.
 Majeshi ya utawala wa Israel yalitekeleza operesheni hiyo kwa kuungwa mkono na serikali za Marekani na Uingereza.
angu mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka uliopita wa 2015 hadi sasa maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu yamekuwa yakishuhudia wimbi la malalamiko ya upinzani dhidi ya siasa za kichokozi za utawala wa Kizayuni na njama za utawala huo za kuvuruga utambulisho wa Baitul Muqaddas pamoja na mpango wake wa kuugawa kiwakati na kimahali msikiti mtukufu wa Al-Aqsa. Wimbi hilo la malalamiko limekuwa maarufu kwa jina la Intifadha ya Quds.
Wapalestina karibu 220 wameshauawa shahidi tangu ilipoanza Intifadha ya Quds mwezi Oktoba mwaka jana hadi hivi sasa.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Masjidul Aqswa ni kibla cha kwanza cha Waislamu na kituo cha mwanzo cha safari ya Mi'iraji ya Mtume Mtukufu SAW, lakini umekuwa ukishambuliwa na kuvunjiwa heshima na magenge ya Kizayuni yenye misimamo mikali huku yakipata uungaji mkono wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Wapigania ukombozi wa Palestina wanasisitiza kuwa, Quds ndio mji mkuu wa dola huru la Palestina litakaloundwa katika mustakabali.
Kishikizo: quds palestina aqsa iqna
captcha